Tanzania Railways Corporation (TRC) to Hire 2,460 Staff for Standard Gauge Railway Project
The Tanzania Railways Corporation (TRC) is expected to hire 2,460 employees for the Standard Gauge Railway (SGR) project on the two sections from Dar es Salaam to Makutopora. This was announced during a two-day site visit by the TRC Board of Directors, which began on August 19, 2025. The visit was to inspect the construction progress of both the SGR and the Meter Gauge Railway (MGR) projects on the Kigoma-Tabora and Tabora-Mwanza sections.
These new positions are in addition to the over 115,000 jobs already created by contractors on the first through sixth phases of the project. The hiring of the 2,460 staff will be implemented in phases. During the 2024/25 financial year, over 500 employees have already been hired. In the current 2025/26 financial year, the plan is to hire 272 staff, with TRC continuing recruitment until the full 2,460 positions are filled.
While this official recruitment by the Corporation is ongoing, the total of 115,000 jobs from contractors has already benefited 115,000 Tanzanians. An analysis of these 115,000 contractor-generated jobs shows that 35,000 are direct employment, while over 80,000 are indirect. These indirect jobs include various groups such as food vendors, motorcycle taxi drivers, auto-rickshaw drivers, and agents for various telecommunications companies.
This job creation fulfills the government's directive that all government-funded projects must benefit Tanzanians, especially those living near the project areas and others, based on required skill levels matching their education and expertise.
Shirika la Reli Tanzania linatarajia kuajiri wafanyakazi 2,460 katika mradi wa reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) kwa vipande viwili vya kutoka Dar es Salaam mpaka Makutopora. Hayo yamebainishwa wakati wa ziara ya siku mbili ya bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) na MGR, kati ya Kigoma-Tabora na Tabora Mwanza liyoanza Agosti 19, 2025.
Ajira hizo ni mbali na zaidi ya ajira 115,000 ambazo tayari zinatokana na nkandarasi katika kipande cha kwanza mpaka cha sita. Katika ajira hizo 2,460 utekelezaji wake ni awamu ambapo katika mwaka wa fedha 2024/25 zaidi ya watumishi 500 wameshaajiriwa na mwaka huu wa fedha 2025/26 tarajio ni kuajiri watumishi 272 na TRC itaendelea kuajiri kufikia watumishi 2,460.
Wakati utekelezaji wa utoaji ajira rasmi za Shirika ukiendelea, jumla ya ajira 115,000 kutoka mkandarasi zimeshawanufaisha Watanzania 115,000. Uchanganuo wa ajira hizo 115,000 kutoka kwa mkandarasi ni kwamba ajira 35,000 ni za moja kwa moja na zaidi ya 80,000 ni zisizo za moja kwa moja zikijumuisha makundi mbalimbali kama mama lishe, bodaboda, bajaji na watoa huduma za makampuni mbalimbali ya mawasiliano.
Utoaji wa ajira hizo ni utekelezaji wa maagizo na maelekezo ya serikali kwamba miradi yote ambayo serikali inawekeza iwe na manufaa kwa Watanzania hususan wale wanaoishi kuzunguka miradi husika na wengine kutokana na ujuzi unaohitajika kwa viwango vya elimu na ujuzi wao.